GET /api/v0.1/hansard/entries/976746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 976746,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976746/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwa hakika, usalama wa nchi hii ni kitu muhimu sana. Ili kupunguza utatanishi na mazungumzo ya hofu nyingi mitaani, ni vyema kabisa tuelezwe kinaga ubaga hali ya usalama ilivyo hapa nchini. Tukiangazia sehemu za kaunti za Wajir na Mandera, tuliona vile mambo yalivyofanyika jana na juzi. Hali ilikuwa ni kulumbana, na watu walikuwa wakifyatuliana risasi hapa na pale. Kunao majangili walioingia sehemu hiyo, ambao sisi tunanona katika runinga na vyombo vingine vya habari, kwamba kuna hali ya kutatanisha katika upande huo. Bi. Spika wa Muda, hali ya usalama sio tu kuhusu bunduki, risasi, kupigana na kulumbana. Hali ya usalama pia inatokea upande was magonjwa, kama vile CoronaVirus Disease (COVID-19). Jana nilipotua katika uwanja wa ndege wa Wilson, mtu alinipima kichwa na kuniambia kuwa niko sawa. Nilipotoka hapo, nikajiangalia na kushangaa kwamba yule alijuaje haraka kwamba niko sawa? Hii ni kwa sababu kwanza sikuwa nimetoka Uchina, bali katika Kaunti ya Tana River, ambako kama ninajua, ni sehemu salama, wala hakuna ugonjwa wa COVID-19. Kwa hivyo, tukishaangalia usalama katika mambo ya kulumbana, twende katika magonjwa kama vile COVID-19, tukienda katika viwanja vyetu vya ndege, ukiteremka tu katika ndege, unapimwa na kuambiwa kwamba joto lako la mwili liko juu ama chini. Sasa, sijajua jinsi gani joto la mwili la mtu linaweza kutambulisha iwapo mtu anaugua ugonjwa wa COVID-19 au la. Sisi tunatoka katika sehemu ya joto katika Kaunti ya Tana River. Kwa hakika, tukiteremka kutoka katika ndege, lazima joto letu litakuwa juu. Ukinipima kisha uniambie, “Joto lako liko juu na unaugua,” basi nitakuwa na wasiwasi. Nikifika kwa mke wangu, nitamwambia, “Nilipofika uwanjani, kuna mtu alinifuata, akanipima kichwani na kitu kama bunduki, na akaniambia kwamba joto langu la mwili liko juu."
}