GET /api/v0.1/hansard/entries/976749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 976749,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976749/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, nimemsikiza vizuri sana Seneta mwenzangu; ni kama anataka kutuletea hali ya taharuki. Hii ni kwa sababu amesema kwamba alipimwa, kisha akaambiwa kuwa yuko sawa; lakini ako na tashwishi iwapo ni kweli ako sawa. Ni vyema basi yeye kuja Bungeni kutuambukiza ugonjwa wa COVID-19, iwapo yeye mwenyewe ako na tashwishi ya hali yake ya kiafya? Kwanza angeenda hospitali iwapo aliona kwamba kile kipimo cha joto la mwili alichopimwa katika uwanja wa ndege hakitoshi. Je, ni njia gani angetumia kujua iwapo yuko sawa bila ya kutoa taarifa Bungeni, kama sio kwenda hospitalini kwanza? Bi Spika wa Muda, tuko na wasiwasi kwa sababu tumekaa karibu sana na yeye; na akikohoa, tutatoroka."
}