GET /api/v0.1/hansard/entries/976757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 976757,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976757/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Nimewasikiza vizuri marafiki zangu, Sen. Sakaja na Sen. Kinyua, ambaye ni Mwenyekiti wangu katika Kamati ya Ugatuzi. Kwa kweli, hali ya kutatanisha ni kwamba ukishuka kutoka kwa ndege, kuna kifaa kinachowekwa karibu na kichwa chako. Sio mimi peke yangu, bali najua kwamba pia hao wamewahi kupimwa hivyo. Wakati unapimwa hivyo, lazima utafikiria, “Alaa, leo unapimwa sehemu yako ya kichwa.” Hii ni kwa sababu mtu anakugusa kichwa hivi. Sasa, anajua haraka vipi iwapo umeambukiwa au la? Katika hali hiyo sasa, lazima kutakuwa na taharuki, mtafaruku na hasa kutatanika hapa na pale. Na jambo hilo sio kwangu peke yangu, bali ni abiria wote walioshuka kutoka kwa ndege. Kama hujawahi kupimwa, jaribu usafiri kesho kupitia uwanja wa ndege wa Wilson au uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, na utapimwa ili ujulikane."
}