GET /api/v0.1/hansard/entries/976758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 976758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976758/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Nikiendelea, Bi. Spika wa Muda, ugonjwa wa COVID-19 ilipatikana Uzunguni, hasa sehemu ya bara Asia kule kwa Wachina. Kule ndiko maafa mengi sana yametokea. Sisi hapa tunatakiwa kuangalia watu waliotoka bara hizo, na hasa kuangalia usafiri wa watu kutoka huko ambao wanakuja upande huu. Katika sehemu ya Kaunti ya Mombasa, mimi sijapata kusikia kwamba kuna COVID-19 Kenya. Iwapo kuna ugonjwa wa COVID-19 Kenya, hatutaki kutatanika wala kuwa na wasiwasi. Bali tunataka Serikali itoe taarifa, iseme iwapo kuna wagonjwa ambao wamepatikana, na kuna hospitali iliyotengwa kwa watu wa ugonjwa wa COVID-19, ili tusitatizike wali kuwa na wasiwasi. Serikali ikifanya hivyo, wale watu waliotuchagua wakituuliza, tutawaambia kwamba kuna hospitali fulani iliyotengwa kwa watu wa ugonjwa wa COVID-19; na kuwa watu kiasi fulani waliolazwa katika hospitali hiyo."
}