GET /api/v0.1/hansard/entries/976777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 976777,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976777/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Bi Spika wa Muda, nami pia nasimama ili kuzungumzia swala la usalama. Ni kweli kabisa kuwa hatuna usalama Kenya, haswa kwenye mipaka yetu. Jana tulionyeshwa kina mama waliokuwa wanakimbia na watoto wakati watu walikuwa wanafyatuliana risasi. Nilipokuwa nikitazama runinga leo asubuhi, kulikuwa na maelezo kuhusu hali ya mipaka yetu katika maeneo ya Turkana na Samburu. Walionyesha watoto wa miaka kumi hivi wakitumia bunduki zilizo na risasi nyingi. Waziri (Dkt.) Matiang’i aliwapa muda warudishe bunduki hizo. Kulikuwa na maandishi kuwa bundiki hizo zinatoka Nigeria na sehemu nyingine. Sijui wanaingilia wapi, ilhali kuna vizuizi kwenye kila mpaka. Hiyo inamaanisha kuwa hakuna usalama hapa kwetu. Inakuwaje watoto wa miaka kumi, kama wale niliowaona wakiwa na bundiki, eti kisa na maana wanalinda ng’ombe wao wasiibiwe ihali wameambiwa wazirudishe? Kuna msemo kuwa ukifunga njia, ufungue njia. Waziri (Dkt.) Matiang’i alisema kuwa bunduki zirudishwe, lakini hatua gani zimewekwa kuhakikisha wale watu wanaacha kuuana na kuibiana? Kama watu hawataacha kuibiana na kuuana, basi watakuwa wakiuana na kuibiana kila wakati, kwa sababu wamekuwa wakipigana tangu jadi. Serikali inachukuwa hatua gani kuhakikisha kwamba kuna usalama kwenye mipaka yetu? Kunafaa kuwe na usalama mipakani ili nasi hapa tuwe salama. Kwa hivyo, naomba Wizara inayohusika na mambo ya usalama ichukue hatua zinazofaa ili kuhakikisha kwamba kuna usalama nchini."
}