GET /api/v0.1/hansard/entries/977181/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 977181,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/977181/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Hapa nimeona - nikinukuu Ripoti kidogo - kuna pahali wamesema kwamba ile miche inatolewa ni kidogo. Inafika kama 100,000 ilhali mahitaji yanafika milioni moja na nusu. Tunaomba wale wanaohusika wahakikishe wamekidhi mahitaji ya wale wakulima. Na sehemu zingine nazo, kila upande wakulima washughulikiwe, kama mfano upande wa ukuzaji pamba. Kuna ukulima wa pamba ambao pia unatusaidia. Mambo ya Blue Economy katika bahari pia yaangaliwe. Kila mtu akifanya bidii upande wake, itatusaidia na tutaweza kujitegemea na tupunguze mambo ya mikopo. Kwa hivyo, Bi. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono na ninatarajia kutakuwa na mabadiliko. Asante."
}