GET /api/v0.1/hansard/entries/977315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 977315,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/977315/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana Bw, Spika kwa kunipa fursa hii. Kusema kweli, ilikuwa jambo la kusikitisha sana kuona ndege kutoka China imetua nchini mwetu. Watu wengi sana wamekuwa na mshangao na wasiwasi. Nawakilisha Kaunti ya Kwale ambapo kuna Wachina wengi wanaotengeneza barabara kutoka Bwego mpaka Vanga. Barabara ingine inayotengenezwa na Wachina ni ile ya kutoka Dongo Kundu mpaka karibu na Ng’ombeni. Ikiwa sisi viongozi hatutapiga kelele kuhusu maradhi haya na serikali kuchukua hatua, tutapoteza watu wetu wengi sana. Nina wasiwasi kwasababu naona athari ya Kaunti yangu ya Kwale. Barabara ya kuenda Kinango inatengenezwa na Wachina hivyo kuna Wachina wengi sana katika Kaunti ya Kwale. Naomba serikali ichukue hatua kwa haraka sana kuhusu maradhi haya ambayo ni hatari kushinda hata Ukimwi. Virusi vya Corona vina ua kushinda ukimwi. Ukipatwa na maradhi haya, unakufa baada ya masaa macheche. Bw. Spika, naunga mkono taarifa iliyosomwa na Senata wa Kaunti ya Narok. Naomba Serikali ichukue hatua kali sana. Wachina ni wengi sana kama watoto katika Kaunti ya Kwale. Maradhi kama haya yakiingia katika Kaunti ya Kwale, tutapoteza watu wengi sana. Naomba Serikali iwakague hawa Wachina wanaofanya kazi katika kaunti zetu ili kuzingatia usalama wa wananchi wetu. Asante sana, Bw. Spika."
}