GET /api/v0.1/hansard/entries/978264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 978264,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/978264/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumpongeza Mhe. Keter kwa kuleta maoni na fikira za vijana katika Bunge Hili. Hakika, kama taifa tunalo tatizo kubwa. Tangu enzi za hayati Mzee Jomo Kenyatta, hayati Daniel Toroitich arap Moi, Rais Mstaafu Mwai Kibaki na sasa, Rais Uhuru Muigai Kenyatta vijana wamekuwa ni wakupewa ahadi kwa midomo tu wakati ambapo wanatakikana kutimiza malengo ya watu fulani. Asilimia sabini na tatu ya wakenya ni vijana. Ni dhahiri hiyo asilimia sabini na tano haionekani. Kuingia katika Bunge hili, kupata kazi na kutafuta riziki katika Jamhuri ya Kenya imekuwa ngumu sana kwa vijana wetu. Hii ni kwa sababu ya sheria ambazo hazina huruma kwa vijana. Ni sheria ambazo badala ya kuwalinda, zinaweza kuwaangamiza. Chukulia mfano wa suala la kuteua mwakilishi wa vijana katika taifa hili. Si vyema Waziri aachiwe jukumu hilo. Inafaa vijana waachiwe jukumu hilo ili wajiteulie wenyewe na waangalie ni kijana yupi ataweza kuzungumzia maslahi ya vijana. Katika Bunge hili, vijana ni wachache. Wale wanaorudi mwaka nenda mwaka rudi ni makaburu weusi ambao wamekataa kuachilia nafasi kwa vijana. Na taswira hii haihusu Bunge peke yake, inahusu taasisi zote katika Jamhuri ya Kenya wakati nyadhifa mbali mbali za uongozi zinapotolewa. Wakionekana kule mitaani ama wanapoomba kazi, sura za vijana kwa Serikali ya Jamhuri ya Kenya ni sura za uhalifu. Vijana wengi “wanapotezwa”. Vijana wengi wanauawa kwa sababu hawapewi nafasi ya kujiendeleza. Katika masuala ya kikazi, hawawezi kupewa kazi kwa sababu kupata nafasi ya kazi ni sharti uwe mjuzi wa kazi hiyo. Utakua vipi mjuzi kama hupewi nafasi hiyo? Kwa mfano, Wabunge wengi wachanga walio katika Bunge la Taifa hawajawahi kuwa Wabunge lakini kwa sababu ya kukataa na kupinga dhuluma za hapo awali, waliweza kusimama kidete na kufika katika Bunge hili. Kwa hivyo sisi ujuzi tunaupata ndani ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}