GET /api/v0.1/hansard/entries/978266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 978266,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/978266/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, Independent",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Jambo lingine ni kuhusu masuala ya elimu. Ningependa kumkosoa Prof. Magoha kidogo na kusema kwamba ukiweka akili yako katika vyuo vikuu sana na usahau kuwekeza katika vyuo vya anuwai, basi kutakuwa na matatizo chungu nzima. Mimi siwezi kuwa profesa. Sote hatutoshi kuwa maprofesa. Sote hatutoshi kuwa madaktari au wahandisi. Kuna wale wanaoongozwa na talanta ya Mwenyezi Mungu. Wengine wamepewa talanta ya kucheza mpira, wengine wamepewa talanta ya kuimba, na wengine wamepewa talanta ya kufanya sarakasi. Ni sharti tutoe nafasi hizi kwa vijana ili waweze kukuza talanta zao."
}