GET /api/v0.1/hansard/entries/978267/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 978267,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/978267/?format=api",
    "text_counter": 277,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Vikwazo ambavyo vimewekewa vijana – masuala ya vyeti vya kuthibisha tabia njema, KRA PIN, CRB, EACC, na hata ada ya kupata leseni kutoka NTSA ya Ksh3,000 – inakuwa ni kama dhuluma na kejeli kwa vijana. Ninapotazama siasa za nchi zinavyoenda na kuangalia masuala ya BBI, ambayo inasema ni kuwaleta Wakenya pamoja, hamna mtu ana pingamizi nalo lakini ukiangalia misafara ya BBI, hamna sauti ya vijana, ambao ni asilimia 73 ya Wakenya wote. Hamna sauti ambayo imekwa pale ya kusema itazungumzia masuala ya vijana peke yake. Building Bridges Initiative itatumia vijana kuwasilisha hoja yao na matakwa yao lakini itahakikisha kwamba hao hao vijana, ambao ni idadi kubwa zaidi katika nchi hii, hawataweza kupata nafasi. Pesa kwa vijana ni suala lingine. Katika Eneo Bunge langu la Nyali kuna pesa ambazo zimetengewa vijana lakini vijana kuzipata ni vigumu sana kwa sababu ya masharti, wizi na ufujaji wa pesa hizo. Dhambi zilizotekelezwa na vijana hapo awali zinabandikwa vijana wa sasa. Ukienda kuomba pesa za vijana, unaambiwa: Kuna wale ambao hawajalipa deni, wakilipa ndiyo tutawapatia. Ni kana kwamba pesa hizo zinatumiwa na watu fulani ambao si vijana – zinawafaidi watu ambao rika yao imepita rika ya vijana. Kwa hivyo, matatizo yote tunayowaletea vijana ndiyo yanayosababisha nchi hii kuenda segemnege. Leo kuwa kijana ndani ya nchi hii ni dhambi. Tukipatikana usiku au mchana, sura zetu zinakaa sura za wezi kwa sababu hatuna kazi, tuna njaa. Tumeponzwa na Serikali, hatupewi lolote. Kila kijana atakayeonekana mitaani anaonekana kama mhalifu – mwizi, muuaji. Hakuna mtu atatizama kijana na sura ya huruma na kusema kwamba huyu kijana hajapata jambo fulani, ndiyo maana yuko mahali alipo. Leo zawadi tunayopata katika nchi hii ni kuuwawa. Ukiangalia wanaopigwa risasi na polisi ni vijana. Waliojaa katika jela zetu ni vijana. Wanaodhulumiwa kila siku ni vijana. Ni kwa nini nchi hii isiweze kutatua shida ya vijana mara moja kwa kuhakikisha kwamba vijana wanapewa zabuni katika taifa hili? Tenders, kama munavyoziita kwa lugha ya kimombo, hazipewi vijana kwa sababu watu fulani wanaamini kwamba kijana akipata maarifa zaidi yako atakuja kukukalia na kufanya mambo ya ajabu. Hizi zabuni zinawekwa kila siku kwa magazeti. Zinatangazwa kwa mdomo tu lakini vijana wa Jamhuri ya Kenya hawapewi nafasi hizi na Serikali ya nchi."
}