GET /api/v0.1/hansard/entries/979075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 979075,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/979075/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie. Mwanzo ningependa kupongeza Kamati kwa kazi nzuri iliyofanya. Wabunge waliotangulia wamezungumzia kwa hamasa kuhusu wakimbizi wa ndani kwa ndani waliofurushwa au kukimbizwa almaarufu kwa lugha ya kimombo kama IDPs. Ni vizuri wale waliofurushwa kutoka mahali walikokuwa wakikaa warejeshwe na haki zao zitimizwe. Sisi wengine tunasikitika tukiona haya. Tunasikitika kwa sababu ni kama Kenya hakujawahi kuwa na wengine kabla ya hawa. Sehemu zingine kukitokea mambo kama haya, hazionyeshwi na hazichukuliwi kwa uangalifu zaidi. Tukiangalia historia, waliofurushwa wa kwanza Kenya ni watu kutoka Lamu wakati wa “Shifta War”. Lamu ina miji tisa; nakumbuka mingine na mingine nimesahau. Kuna Mvundeni ambao sasa haupo, Rubu na Mwambore. Kuna miji tisa. Ilibidi watu wakimbie miji hiyo kwa sababu ya idhilali walizozipata wakati mashifta walipokuja. Watu walinajisiwa. Walipigwa na hata walipokonywa mali yao. Ilibidi wakimbie The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}