GET /api/v0.1/hansard/entries/979076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 979076,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/979076/?format=api",
    "text_counter": 282,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "wakaishi vijiji vingine. Watu hao walikimbilia Kisiwa cha Pate, Lamu, Mkokoni, na Kiwayu. Walifika mwambao wa Pwani, Malindi na Ngomeni. Wabajuni wako sehemu hizo zote kwa sababu walifurushwa makwao. Hakuna mahali mtasikia wao wamepangiwa nini. Kile tunachosikia ni kuhusu waliofurushwa huku. Kule Lamu hakuna kinachozungumziwa. Nalileta hili nalo lijulikane kwamba kuna Wakenya wengine waliopata idhilali hizi na mambo yao yanafaa kuangaliwa. Kama ni kurejeshwa, pesa iliyoko ipangiwe pia wao. kulingana na Ripoti, pesa iliyotolewa ya kununua ardhi ijumuishe pia watu wa Lamu kwa kuwa wao pia ni Wakenya. Sharti wajenge mashule na miji yetu irudi. Mimi ni mmoja wao. Nyanya zangu waliofukuzwa huko ikabidi tukae sehemu nyingine. Hata hivyo, huko hakutajwi. Kunatajwa sehemu zingine tu. Katika hii Ripoti nimeona wanazungumzia maji. Maji ni uhai. Ningependa tena kuipongeza Kamati. Nasikia walizunguka na wakafika hata Lamu. Kamati ilitembea sehemu za Bargoni. Ilikuwa kujengwe kidimbwi cha maji. Pesa nyingi zimetumiwa lakini ukitembea kule hakuna kitu kule mashinani; utaona tu kwa vitabu. Ninawapongeza hata Auditors. Kwa lugha ya Kiswahili wanaitwa wahakiki. Wahakiki hawa wamefanya jambo la maana maanake wakienda sehemu kama za Lamu, hawatapata kufanya kazi zao vizuri. Wataambiwa sehemu hizo kuna Al-shabaab . Watakwamia hapo Lamu Town kisha hawataenda mashinani. Wakienda mashinani, watagundua kuna matatizo mengi. Wao ndio wanaoweza kufanya wananchi wapate huduma bora. Kwa hivyo, hili jambo la maji naomba Kamati iliangalie vizuri. Kuna miradi mingi kama huo mmoja wa Bargoni. Kuna shida ya maji na ni jamii iliyotengwa. Pesa zilitengwa na serikali na mradi haukufanywa. Watu wamezungumzia ile pesa inayojulikana kama Equalisation Fund. Kusema kweli, pesa hiyo itatusaidia sisi watu tuliotengwa. Lakini kama hao wanaona—naona Wabunge wenzangu wanaipigania sana ipelekwe sehemu zao—hatukatai ipelekwe, lakini mwanzo mhakikishe kule kwetu tuna stima kila pahali kama kwenu, tuna barabara, shule na vitu vyote. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}