GET /api/v0.1/hansard/entries/980040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980040,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980040/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Mimi naunga mkono hii bodi iweko. Watu labda watashangaa kwa nini nasimama hapa kuchangia mambo ya chai, lakini sisi ni wanyuaji chai Lamu, na wanaopanda ni Wakenya. Tunafaa kuwaunga wenzetu wapate kutengeneza chai nzuri. Sisi watu wa Lamu ndio tunaipika chai kushinda wao wanaoipanda. Na tunaipika vizuri. Kuna hoteli fulani Kenya inajulikana ukienda Lamu uinywe chai yake ni chai spesheli. Ukienda kama Mangroove Lamu uende Mwanaratha, msitoke Lamu bila kununua chai huko. Ni chai tamu. Chai spesheli. Ni chai ya kukumbukwa. Pia ningependa watakaotekeleza mambo haya wakumbuke pia kuna mimea mingine sehemu zingine. Kwenye ukanda wa Pwani, mumea unaotuletea pesa ni mkorosho. Kwa hivyo mkorosho pia utengenezewe bodi yake. Kuna mkorosho wa kisasa aina ya grafting, ambao huzaa korosho nyingi. Tunataka wakulima wapewe mikorosho aina hiyo mingi ili wapate kuwa na korosho nyingi ili Kenya ipate kujitegemea vizuri. Pia, kuna shirika la Kenya National Cereals and Produce Board (KNCPB), ambalo tunaliona linafanya kazi vizuri katika sehemu zingine nchini. Tunataka pia wajue kwamba katika sehemu ya Mpeketoni tunapanda mahindi, na wakulima huvuna magunia ya kilo 90 zaidi ya 40,000. Tunataka shirika la NCPB lije kule lifanye kama linavyofanya kwingineko. Shirika hilo likinunua mahindi hayo litakuwa linawaondolea mzigo wakulima. Wakulima wa mahindi kule Mpeketoni wanalima kwa umaskini; hakuna msada wanaopata kutoka kwa Serikali. Kwa hivyo, shirika la NCPB lije kule ili wakulima wapate moyo wa kufanya bidii zaidi. Wakulima katika sehemu zingine, kama vile Basuba, watapata moyo wa kupanda mahindi kwa wingi ili tujitegemee Lamu. Kule Lamu kuna sehemu ambako wakulima wakipanda mahindi wanapata mazao mazuri. Watu wasifikirie kwamba Lamu ni upande wa samaki pekee, na upande wa mahindi watuwache nyuma."
}