GET /api/v0.1/hansard/entries/980041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980041,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980041/?format=api",
    "text_counter": 287,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Pia, kama nilivyotangulia kusema kwamba Lamu watu wanatujua kwa samaki, watu wakizungumzia chai pia sisi tuzungumzie samaki. Upande wetu wa Lamu tunaomba wajitokeze kwa zaidi, wanaohusika waje watusaidie manake watu kule ni watenda kazi, hakuna uvivu. Watu wanajitahidi. Wavuvi wamejitahidi wanawasomesha watoto wao kwa hizo hizo pesa za bahari, pesa za shida. Lakini kuna uvuvi wa kisasa. Serikali ije ipeane vifaa vya kisasa ili wavuvi wapate kwenda kwenye bahari kuu. Kwa saa wanang’ang’ana na bahari ya ndani. Tunaomba wavuvi wasaidiwe na vifaa kama vile vifaa vya GPS na vifaa vya kutafuta samaki, kwa lugha ya kimombo vikijulikana kama fish finders . Tunataka wapewe vifaa hivyo ili waweze kuleta samaki wengi. Samaki bado wana soko hadi sasa. Samaki wengine wanatoka China wanaletwa Kenya na sisi tunayo Bahari ya Hindi, ambako tunaweza kutoa samaki mpaka tukauze nje."
}