GET /api/v0.1/hansard/entries/980149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980149,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980149/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Bw. Spika, kuna matamshi mengine ambayo mtu akiyatamka, anavunja watu mioyo. Mfano ni kusema kwamba hao nzige wamegeuka rangi ya dhahabu ama samawati na kwa hivyo watakufa. Kwa mfano, kuna Maseneta wanawake na wanaume. Watoto wenu wadogo wanawaona kama ‘mungu’ wao. Hata wakipigwa na mtu au hata wakitukanwa, wanasema: “Baba akija---” Anajua baba yake hawezi kufanya kitu, lakini baba yake kwake ni ‘mungu’ wake; anaamini kuwa anaweza kila kitu. Sasa sisi na wananchi tunamtegemea Waziri wetu kama baba anayeweza kila kitu. Lakini sasa akijitokezea na kuzungumza maneno aliyozungumza, ni kumaanisha kwamba huyu baba hawezi kutegemewa na inavunja mioyo vibaya sana. Hata kama naweza kufa kesho, ukinitia moyo na kuniambia, “mimi naona hufi, hata mimi nilikuwa hivi na nikapona,” unanipa maneno ya faraja. Lakini huyu anavunja moyo na kutuonyesha kwamba hana la kufanya kuhusu hawa nzige. Bw. Spika, una jambo la kufanya. Mahali ilipofika sasa, sio jambo la mchezo tena. Hii ni kwa sababu mwaka uliopita, Mwenyezi Mungu alitujalia mvua na tukapata vyakula vingi sana. Lakini sasa, tumerudi pale pale kwa kulia. Vijana wetu hawana kazi, kuna athari ya Corona Virus na kuna ukosefu wa chakula. Sasa tutatatua shida ipi na kuacha ipi? Huu ni mchanganyiko moja kwa moja. Biblia inasema, “watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.” The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}