GET /api/v0.1/hansard/entries/980223/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980223,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980223/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Bw. Haji, Afisa Mkuu was HAKI Africa na mimi tulizungumzia jambo hili wakati mmoja huko Pwani. Ijapokuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma alihuzunishwa na jambo la mauwaji ya kiholela, hajaweza kufanya jambo lolote kuhakikisha haki za Wakenya zinalindwa. Jambo la kuudhi kabisa ni kwamba vyumba vya kuhifadhi maiti ambako wahusika wa mauwaji hupelekwa, hulipisha familia za waliowaawa hela mingi ilhali familia hizo hazijui waliotekeleza mauwaji hayo."
}