GET /api/v0.1/hansard/entries/980781/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980781,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980781/?format=api",
    "text_counter": 34,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kujiunga na wewe kuwakaribisha waheshimiwa waliofika hapa kutoka Bunge letu la mashinani la Kisii. Ninaimani kwamba muda ambao wametumia hapa kujifundisha na kujionea, watarudi nyumbani ili wakaweze kuendeleza Kisii County kwa yale mafunzo waliyoyapata hapa. Hapa Seneti tunajivunia jabali mkongwe wa kisiasa aliyekomaa kisawasawa ambaye sisi tunamsifu sana, Sen. (Prof.) Ongeri, kwa uhudumu wake wa kuhudumia watu wa Kisii katika Seneti. Kitu ambacho nataka kuambia Waheshimiwa ni kwamba Katika zile kura sita mlizopiga, kama kuna moja muhimu mliyofanya, nyinyi kama wabunge wa Kisii, ni kura ya kumpigia Sen. (Prof.) Ongeri. Bw. Spika, najiunga na wewe kuwakaribisha na ninahakika kuwa watakaporudi nyumbani watakuwa wamejionea wenyewe kwamba hapa hata akina mama walioko hapa tumewapa vyeo kama wenyekiti na naibu wenyekiti. Kwa mfano, Sen. Dullo ni Mwenyekiti wa Managed Equipment Services (MES), special Committee ambayo ilitengenezwa na Senate. Vile vile, yeye ni wakili na naibu wa Kiongozi wa Walio wengi Katika Senate. Kwa hivyo, ninahakika kuwa watakapo rudi nyumbani, dada zetu wengine watapewa nafasi waweze kuchukua nyadhfa kama hizi. Asante."
}