GET /api/v0.1/hansard/entries/980859/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980859,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980859/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Sasa katika yote tunayozungumza, ni mikakati gani ambayo imewekwa kuona kwamba ugonjwa huo utakapoingia humu nchini, utakabiliwa vilivyo? Iweje basi Mchina akitoka kwao na aingie hapa nchini awe hana huo ugonjwa lakini Mkenya aliye China akirejea hapa nyumbani awe nao? Kama Wakenya walisema ndege zao zisiende China, sawa. Je, walikataza za China kuingia Kenya? Kama hawajakataza, lengo na madhumuni yao ni nini? Wale walio kule China ni watoto wetu tuliozaa sisi. Mwenyezi Mungu aliweka siri kwamba hakuna anayejua atakufa lini. Kuwaacha watoto wetu wakae kule China ni sawa na kuwahukumu wafe. Tumeshawatoa kafara. Kama mzazi, mimi naona tunapoteza. Balozi wetu kule China hafanyi kazi yake vilivyo. Hii inamaana kwamba anazingatia tu biashara kati ya Kenya na China. Ni lazima pia aangalie maswala ya watu wetu walio China. Ni hatua gani amechukua kuhakikisha kwamba watu wetu kule China wamewekwa mahali salama na kuwa wanapata chakula na mahitaji mengine ya lazima? Bw. Spika, Biblia inasema kwamba imani isiyokuwa na matendo imekufa. Sasa hata akizungumza na hachukui hatua yoyote, hatusaidii bali anatuongezea mashaka. Tuna tashwishi na Wizara husika kwa sababu hapa nchini hata ukipata malaria unaaga. Ukimwi ulikuja tukaambiwa unaitwa ukimwi. Sijui jina hilo lilitoka wapi. Vile vile, kumekuja Corona Virus . Hatujui jina hili limetoka wapi. Ugonjwa kama haujulikani mbona majina huwa yaja? Je, jina hili lilitengwa ili ugonjwa huu ukitokea utapewa jina? Hii njaa yetu ndogo itafanya tumalizike kama Waafrika ama Wakenya. Ombi langu ni kwamba Wizara husika ifanye mikakati inayowezekena; aidha kuwaleta Wakenya waliyo kule China hapa au kuhakikisha usalama wao. Pili, tuhakikishe kuwa ndege za China haziingii nchini. Hii ni kwa sababu hao pia ni binadamu kama sisi na wanaweza kushikwa na maradhi. Ikiwa watoto wetu hawarudi hapa, basi hata wao pia wasiruhusiwe kuingia. Bw. Spika, tunataka kuona hatua zinachukuliwa kuhakikisha Wakenya ambao wako kule China wametunzwa huko iwapo hawawezi kurudishwa hapa. Serikali ichukue hatua kuhakikisha wanalindwa kwa sababu wakiwa kwa shida, sisi kama wazazi huku pia tuko kwa shida."
}