GET /api/v0.1/hansard/entries/980863/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980863,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980863/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13156,
        "legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
        "slug": "mutula-kilonzo-jnr"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Wamesema nizungumze Kiswahili. Jambo hili linatutatiza sisi Wakenya. Mimi nimepigiwa simu na watu wawili kutoka Kaunti ya Makueni ambao wanasoma kule China. Mmoja wao ni profesa. Wanasema kwamba wanahofia kuwa maradhi hayo yatawakabili sehemu wanayoishi. Ukweli ni kwamba Wizara husika haiwezi, haitawahi, haijui na haitawajibika. Mheshimiwa Rais anafaa kujitokeza na kukipa swala hili kipau mbele. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ambako ndege zinatua, kunapaswa kutengenezwa hospitali maalum. Mimi nilishangaa kusikia ya kwamba wametenga vitanda katika hospitali ya Mbagathi. Vitendawili vya Kenya havitawahi kuisha. Yaani, huyu ni mtu ambaye haelewi. Mtu ambaye anasemekana kuwa na ugonjwa huu, sijui ni Corona au Corolla --- Sen. Gona ameuliza swali la maana sana. Kwa nini ugonjwa huu umeitwa ‘ Corona ’ na si ‘ Corolla ?’ Wametenga vitanda katika hospitali ya Mbagathi, lakini hawajui mtu atatoka upande gani. Jana nimepata ripoti katika mitandao ya kijamii na nikamwelekeza Kamishna wa Kaunti ya Makueni achukue hatua. Ripoti yenyewe ni kwamba kuna Mchina ambaye amewekwa kule Thwake, Kaunti ya Makueni na anaonekana kuwa na virusi vya Corona . Mwingine anasemekana kuwa katika Kaunti ya Kitui. Bw. Spika, juzi nikitembea mtaani nilimuona Mchina amejifunga kana kwamba ana virusi vya Corona ."
}