GET /api/v0.1/hansard/entries/980872/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 980872,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980872/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": "Ndege wa Wilson tulikutana na watu walikuwa na vifaa kama bunduki. Walikuwa wameweka kifaa kingine kichwani na sikujua wanaangalia nini. Hata hivyo, Sen. Shiyonga amesema kwamba si lazima watu wanaoweza kuwa na Virusi vya Corona wapitie katika uwanja wa ndege. Wanaweza kupitia Lunga Lunga kwa Sen. Gona au hata Ziwa Victoria. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Wakenya kujua kwamba afya yetu inaangaliwa. Bw. Spika, je, mtu mmoja akipatikana na ugonjwa wa Corona katika vitongoji duni kama vile Kibera, Mathare au Kawangware, tutafanya nini? Je, tutaifunga hii nchi ili mtu asitoke kama walivyofanya Wuhan? Jambo hili halifai kuchukuliwa kwa urahisi vile linavyochukuliwa. Jambo hili si mzaha. Sisi viongozi hata kuanzia wikendi hii, tukienda kujenga madaraja ya kufanya Kenya iendelee mbele, yaani BBI, tuzungumzie jambo hili. Tumwambie Mheshimiwa Rais tusimamishe mambo ambayo tunafanya na tuhakikishe watu wako sawa. Mimi ninahofia siku ile itasemekana mtu ameanguka katika Barabara ya Tom Mboya na ana virusi vya Corona . Mungu atusaidie. Kama vile Balozi Serem alivyosema, kama si Mungu, mimi sijui tutafanyaje katika nchi."
}