GET /api/v0.1/hansard/entries/980884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 980884,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980884/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Pia mimi ninaunga mkono Taarifa hii. Ninafikiria imekuja kwa wakati muafaka. Virusi vya Corona ni virusi ambavyo vimekua kama donda ndugu katika maisha ya Wakenya. Hii ni kwa sababu huwezi kujua tofauti kati ya wanaougua na wasiougua hivi virusi. Hivi sasa, kuna watu wamewekwa mahali ili kuchunguza kama wana huo ugonjwa. Kuna tashwishi kwa sababu ni kama siri inafanyika. Mpaka sasa, Kenya haijachukua msimamo kabisa kuwa wale waliochunguzwa wameingia wengi na wametoka wengi. Hakuna hata mmoja amesema amepatikana na Virusi vya Corona. Kwa hivyo, inaonekana kuwa kuna sababu fulani ya sisi kutoambiwa ukweli kuhusu janga hili. Rais mwenyewe alimfuta kazi yule Waziri wa Ukulima na akamhamisha Waziri wa Afya na kumchagua Sen. Kagwe achukuwe mahali pake. Ni sawa kabisa kufanya marekebisho, lakini kama yule Waziri hawezi kazi, ni vyema kumwachisha kazi kuliko kumpeleka kwingine aende aharibu vile vile. Tunajua kwamba Kamati ya Seneti inachunguza mambo ya Medical Equipment"
}