GET /api/v0.1/hansard/entries/980886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980886,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980886/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": ", ambayo imekua mess kubwa zaidi katika hayo maneno. Kwa hivyo, ikiwa Kenya haiko tayari kuangalia Virusi Vya Corona na kuangalia maneno yanayokuja, sababu zingine ni kama hizi. Mawaziri wengine wanazembea kwa kazi zao. Bw. Spika, mimi ninajua kuwa umesafiri sana na umefika sehemu mbali mbali za Kenya. Utaona kwamba ukiwa huko Mandera - na ninajua kuwa ndugu zetu wanatoka sehemu hizo - ni lango la kuingia na kutoka haswa kwa watu wanaotembea. Utashangaa kuwa lango liko wazi. Ukitoka Kenya kuenda Somalia ama kutoka Somalia kuja Kenya, unaweza kupita bila mtu yeyote kukuuliza unaenda wapi. Kwa hivyo, si mambo ya kusafiri na ndege pekee. Ukifika uwanja wa ndege, kifaa kama bunduki kinawekwa kinaelekezwa kwenye kichwa chako halafu unaambiwa kuwa huna virusi. Tukiwa watu wa ukweli, Wizara ituambie kama ugonjwa huu uko Kenya ama hapana. Watupatie hesabu ya watu walioambukizwa na wasioambukizwa kwa sasa. Mimi ninaona kuwa Wizara ya Afya ndio ina jukumu kubwa kuangalia afya yetu. Serikali ni lazima ichukue msimamo ambao utatetea afya ya Wakenya kupitia Wizara ya Afya. Mwisho, ni jambo la aibu kuwa kuna Wakenya waliozuiliwa na Serikali ya Uchina. Mpaka hivi sasa, Serikali yetu haijachukua msimamo kutamka lolote kuhusiana na Wakenya waliozuiliwa kwa sababu walipatikana na Virusi vya Corona."
}