GET /api/v0.1/hansard/entries/980900/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 980900,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980900/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa na Sen. Kwamboka na mwenzake, Sen. Kasanga. Nawapongeza Maseneta wote ambao wamechangia taarifa hii kwa lugha ya taifa, Kiswahili. Wengi wemeweza kuzipata hisia za Wakenya kwamba swala la Virusi vya Corona ni swala linalotamausha Wakenya wengi. Kuna mipaka mingi katika nchi yetu ya Kenya inayotumiwa kuingia and kutoka. Kwa mfano, kuna mipaka kule Turkana, Bungoma, Mt. Elgon, Busia, Lamu, Mandera, Garissa, Lunga Lunga na kwingineko kwingi ambako watu huingia na kutoka katika nchi ya Kenya. Je, kaunti zetu zimejitayarisha vipi kupambana na swala hili? Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wasafiri wanapimwa joto kutumia kipima joto linalowekwa kwenye kwapa. Maoni yangu ni kwamba wanafaa kupima wasafiri iwapo wana dalili zingine za Virusi vya Corona kama homa. Bw. Spika, Kamati ya Afya lazima izingatie jambo hili kwa sababu ni swala linalohusiana na maswala ya afya. Nchi yetu ya Kenya haijajitayarisha kupambana na Virusi vya Corona . Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii."
}