GET /api/v0.1/hansard/entries/980933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 980933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/980933/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninampongeza Sen. Iman kwa kuleta maombi haya kwa Bunge la Seneti. Hili ni swala nzito sana kwa watu wa North Eastern kwa sababu swala la Al Shabaab ni la kitaifa. Si la jamii moja ama eneo moja. Uamuzi wa kwenda Somalia kupigana na Al Shabaab haukufanywa na watu wa North Eastern. Ulifanywa na Serikali ambayo iko Nairobi. Leo Serikali ile imeamua kuondoa walimu kutoka eneo lile ili wanafunzi wasiweze kusomeshwa. Je, ipo haja ya hili swala la uajiri wa waalimu lipelekwe Mashinani ili kila kaunti iwe na tume yake ya kuajiri walimu; waweze kufanya uchunguzi wa walimu wanaotaka kuajiri ili waweze kuajiriwa?"
}