GET /api/v0.1/hansard/entries/981070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 981070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981070/?format=api",
    "text_counter": 323,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kumuunga mkono ndugu yangu, Sen. M. Kajwang’, ambaye pia ni mdogo wangu. Hii ni kwa sababu ameleta Mswada huu ambao ni wa maana sana, unaohusu mambo ya uchukuzi, ufugaji na biashara ya samaki. Nimetafakari mageuzi haya na nikaona kuwa yako katika mstari wa mbele. Kitu muhimu cha kunakili, ni kwamba hakuna chochote kinachotengenezwa cha samaki kisichohusu mvuvi. Mimi natoka katika eneo la Pwani. Ufuo wote wa Pwani ni ufuo wa bahari. Wengine wetu tulisomeshwa na wazee wetu kutokana na mapato ya uvuvi wa samaki. Vile vile, tuko na maziwa kama matatu hivi yanayojulikana Kenya. Ziwa kubwa katika Afrika nzima ni Ziwa Victoria. Ndugu yangu, Sen. M. Kajwang’, anatoka katika sehemu hiyo. Lakini hiyo sio sababu pekee ambayo imemfanya kuleta Mswada huu. Watu wa Turkana pia wana Ziwa Turkana, na kuna maziwa mengi nchini Kenya. Hata wale watu wanaoishi kando ya mito ni wafugaji wa samaki. Ikiwa wataweza kupata samaki, watayarishe na wauze au watengeneze mpaka ile minofu ambayo huwekwa kwenye pakiti baadaye na kuuzwa ng’ambo--- Ukienda katika mitambo ya kutengeneza ngozi ya samaki kule Kisumu, utaona kuwa kuna maarifa mengi yanayotakikana. Kwanza, kuna kupara ngozi, ambayo inatengenezwa sawa sawa na kuwekwa katika paketi na kupelekwa ng’ambo."
}