GET /api/v0.1/hansard/entries/981081/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 981081,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981081/?format=api",
    "text_counter": 334,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia pendekezo la mabadilisho ya sheria ya uvuvi, usimamizi wa uvuvi na utekelezaji wake. Mswada huu umekuja katika wakati mwafaka. Tumeona uchumi wa Kenya umekuwa ukiregerega kwa sababu ya zile nyanja tofauti ambazo zinasimamia uchumi wa Kenya zimelemaa katika utendakazi wake. Uvuvi unaweza kutupa fursa nzuri ya kuongeza mapato ya nchi, hususan samaki wale wakitayarishwa na kusafirishwa katika nchi zingine ile wauzwe katika soko za nje. Vile vile, uvuvi unatoa fursa kwa Wakenya kupata chakula ambacho hakina madhara, isipokuwa sehemu za uvuvi ambako maji yameingiliwa na mchafuko kutokana na ‘ contamination ’ ya maji taka au kemikali zinazo athiri maisha ya samaki."
}