GET /api/v0.1/hansard/entries/981083/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 981083,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981083/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, naunga mkono mapendekezo ambayo yametolewa na Sen. Kajwang’, isipokuwa moja inayopendekeza mkurugenzi mkuu kukaa ofisini kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu. Wakurugenzi wengi hukaa ofisini kwa muda wa miaka matatu, na huo umekubalika kama wakati mzuri wa kufanya kazi na kuendelea na mambo mengine. Wavuvi wetu wengi hawana uwezo wa kununua vifaa vya kuwaezesha kuvua samaki katika sehemu za bahari kuu, ambako kuna samaki wengi kuliko mikono ya bahari kama Tudor, Port Reitz na kwingineko. Kwa hivyo, ipo haja ya serikali za kaunti kutoa ruzuku kwa hao wavuvi, ili kuhakikisha kwamba wavuvi wanapata vifaa vya kisasa vya kuwawezesha kwenda katika sehemu za nje, ili wavue samaki wengi na kuinua mapato yao. Bw. Naibu Spika, jambo la pili ni kwamba sehemu nyingi za uvuvi hazina vifaa vya kuhifadhi samaki wale baada ya kuvuliwa. Kwa mfano, mvuvi akienda baharini usiku halafu arudi na samaki wengi, ikiwa hatapata mahali pa kuwahifadhi kwa baridi, samaki wale huharibika, na itakuwa amefanya kazi bure. Kwa hivyo, iko haja pia ya serikali zetu za kaunti kuwasaidia wavuvi, kwa sababu uvuvi na ukulima ni huduma ambazo zimegatuliwa kikamilifu. Ipo haja ya serikali za kaunti kuekeza katika huduma kama hizi, ili kuhakikisha kwamba samaki wanaovuliwa na wavuvi hawapotei. Bw. Naibu Spika, sehemu kama Lamu iko na curfew kutokana na ukosefu wa usalama. Kuna ukosefu wa usalama kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya Al- Shabaab, inayofanya Serikali kuzuia wavuvi kutoka usiku kwenda kuvua au kusafirisha samaki waliovuliwa usiku. Samaki waliovuliwa na wavuvi katika Kaunti ya Lamu wasio kuwa na vifaa vya kuhifadhi samaki wataharibika barabarani wanaposafirishwa ambapo itakuwa hasara kubwa kwa wavuvi. Bw. Naibu Spika, ipo haja ya wavuvi wa samaki kupewa kipa umbele kwa sababu ni njia rahisi ya kukidhi mahitaji ya Wakenya kichakula na kimapato. Unaweza kula samaki kutoka Jumatatu mpaka Jumapili. Kama vile Sen. Madzayo alivyosema, kuna samaki wengine kama vile papa, nguru au jodari. Samaki hao wakubwa wana virutubisho fulani ambavyo husaidia kuwahami wazee, kama Sen. Madzayo, ambao wanapata shida wakati wa baridi na sehemu zingine kuhakikisha wanajenga joto la kutosha mwilini ili wapambane na huduma za kijamii."
}