GET /api/v0.1/hansard/entries/981095/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 981095,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981095/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa kumalizia, Bw. Naibu Spika, hatari nyingine inayowakumba wavuvi katika eneo la Mombasa ni ukataji kiholela wa mikoko. Mikoko huwapa samaki fursa ya kuzaana, na pia kuondoa hewa sumu kutoka katika mazingira na kuleta hewa safi. Mikoko huwa kama misitu inayosaidia kuhami maeneo ya bahari. Wakati mikoko inakatwa kiholela, ina maana kwamba zile sehemu ambazo samaki wanaweza kutumia kutaga mayai zinaharibika, na hatutaweza kupata samaki wengi kama vile ambavyo tungeweza kupata wakati mikoko ile itazingatiwa kulindwa. Kwa hivyo, inamaanisha kwamba iwapo mikoko itakatwa baharini, sehemu zote ambazo samaki hutumia kutaga mayai zitakuwa zimeharibika, na kutakuwa hakuna mahali pa kutaga samaki. Mwisho, Bw. Naibu Spika, ni kwamba kuna swala la uchimbaji katika bahari. Utapata kwamba katika bandari kwa sasa, kwa mfano Kenya Ports Authority (KPA) au lile Shirika la Bandari la Kenya linajenga terminal mpya ya vyombo. Wanatumia mchanga kutoka sehemu kuu ya bahari ambako wanachimba chini. Mchanga ule wanakuja kuujaza ili wapate sehemu ambayo wataweza kujenga terminal ile. Kuchimba huku kunaathiri mazingara ambayo samaki wanatumia kuishi na kutaga mayai. Hii ni kwa sababu wakichimba, zile fujo ambazo zinatokea zinaathiri samaki, kwa sababu samaki hawapendi mazingara ambayo yako na makelele au utatanishi katika sehemu ya bahari. Uchimbaji ule ukifanyika, zile sehemu ambazo samaki wanaweza kupata fursa ya kutaga mayai na pia kukaa kwa utulivu ili waweze kuendelea na shughuli zao, wanakimbia. Ina maana kwamba wavuvi hawataweza kupata samaki wengi kuvua; na vile vile kupata mapato ambayo yatawasaidia kuendesha maisha yao. Bw. Naibu Spika, katika suala hili, pia ni lazima halmashauri ambayo inatarajiwa kusimamia mambo ya uvuvi iyaangalie. Wavuvi wale hawana fursa ya kupata mapato mengine wakati mazingara ya samaki yameathirika. Nafurahi kwa Mswada huu ambao umeletwa na ndugu yetu, Sen. M. Kajwang’ wa Homa Bay. Hii ni kwa sababu pia kule, uvuvi wa samaki ni jambo kubwa sana. Wiki iliyopita nilikuwa katika maeneo ya Bondo, Rongo na Kisumu, na chakula changu kingi kilikuwa ni samaki. Kwa hivyo, tunaomba kwamba Mswada huu upitishwe."
}