GET /api/v0.1/hansard/entries/981552/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 981552,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981552/?format=api",
    "text_counter": 362,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "kama makaa. Huwa wanamwaga mbegu zao na wanawacha hapo chini. Saa hii tumeshtuka sana kwa sababu nzige hawa wana ugonjwa ambao tunaogopa hata sasa. Mara ya kwanza walipomwaga dawa hiyo, haikuwaua wale nzige. Badala ya kufa, wakaanza kushuka chini na kufagia kila kitu vile ambavyo trekta hufagia. Hutaona nyasi hata moja. Ni jambo ambalo litaleta shida katika Kenya nzima kwa sababu nzige wanahama na yale mayai yamemwaga pale ndiyo yanaamka. Naomba Serikali iamke na kuangalia ile dawa inamwagwa kwa sababu isipopimwa vizuri, tunaogopa kuwa italeta shida. Pahali ambapo dawa inamwagwa hapa chini panakauka. Nyasi inakauka. Tuna shida na ni lazima iangaliwe. Hao nzige watatembea kila pahali ambapo kuna joto. Tuna hakika watafika Turkana na pande zingine kwa sababu wanatambaa pahali kuna joto. Naomba jambo hili lichukuliwe maanani kabisa. Serikali ijue kuwa hili ni jambo baya zaidi. Mbeleni, baba zetu walitueleza kuwa wakati nzige walikuja, mahali walilala palichomwa kwa sababu ilijulikana mavi yao italeta madhara kwa ng’ombe na watakufa kutokana na ugonjwa. Jambo hili linafaa liangaliwe badala ya kusema tunangoja dawa itoke sijui wapi. Hawa nzige wanatambaa tu. Hawasimami. Ningependa jambo hili lichukuliwe kama jambo baya litakaloleta maradhi pande zote."
}