GET /api/v0.1/hansard/entries/981570/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 981570,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981570/?format=api",
    "text_counter": 380,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": {
        "id": 13274,
        "legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
        "slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
    },
    "content": " Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa ili nichangie suala la nzige. Kweli mvua ilinyesha na kawaida mvua ni baraka. Tunajua kama Wakenya tumepitia kipindi kigumu awali cha ukame ambapo ilibidi watu wetu waishi kwa kutegemea chakula cha msaada. Basi wakati mvua ilinyesha, watu walijitupa mashambani wakalima kwa bidii. Inaleta wasiwasi sana wakati tunasikia kwamba mazao ambayo tulikua tunatarajia yatavamiwa yataliwa na nzige. Wengine wetu hapa tunatoka sehemu ambayo mvua hiyo ambayo ni baraka iliwadhuru watu kwa sababu kulikuwa na mafuriko na mimea mingi tuliokua tunatarajia ilisombwa. Nikisimama hapa, nzige hawajafika Kaunti yangu ya Taita Taveta lakini sipati usingizi kwa sababu tunatarajia chakula kutoka wenzetu ambao wamevamiwa na nzige. Ndiposa tunasema kwamba jambo hili lichukuliwe kwa dharura kubwa sana. Inatakikana suluhu mwafaka ipatikane kusuluhisha jambo hili la nzige. Naunga wenzangu mkono ambao wameongea awali. Huu ni wakati suala la nzige litangazwe kuwa janga la kitaifa nchini Kenya kwa sababu kupitia mifano nimetoa awali vile watu wamekua wakikosa chakula na vile mvua ilinyesha na hakuna suluhu mwafaka, basi ni vizuri kama nchi tuseme kwamba ni janga la kitaifa ili idara husika ziweke vichwa pamoja ili tuweze kupata suluhu thabiti la kutusaidia kupambana na janga hili. Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie. Nampongeza mwenzangu ambaye ameleta Hoja hii ili tuijadili."
}