GET /api/v0.1/hansard/entries/981642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 981642,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/981642/?format=api",
    "text_counter": 43,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa kuchangia malalamiko ambayo yameletwa na Sen. Anuar. Kwanza, ninachukua fursa hii kumpongeza Sen. Anuar kwa kuleta Ombi hili katika wakati mwafaka ambapo wananchi wengi, husasan katika maeneo ya Lamu, wanapata shida za huduma za afya ambazo ni muhimu katika maisha ya binadamu. Bw. Spika, Lamu si kama sehemu zingine ambapo unaweza kwenda katika kaunti jirani kupata matibabu. Jirani wa Kaunti ya Lamu ni Kaunti ya Tana River ambako kuna shida nyingi zinazohusiana na matatizo ya afya. Kwa hivyo, swala la Lamu linafaa liangaziwe kwa karibu kwa sababu ni shida kupata usafiri wa kutoka mjini au kijijini mpaka sehemu ambapo huduma za afya zinapatikana. Mbali na hayo, majuzi mgonjwa alicheleweshwa kufikishwa hospitalini na hali yake ikazorota alipokuwa anatoka Lamu kuelekea Mombasa kwa sababu gari halikuwa na mafuta. Kwa hivyo, hili ni swala ambalo lazima tuliangazie kwa makini zaidi kwa sababu Lamu si kama miji mingine; ni sehemu ambayo iko katika upembe wa Pwani. Hivi sasa, Kaunti ya Lamu imekumbwa na matatizo ya kiusalama. Majuzi, watu walivamiwa na wengine wakapoteza maisha na kujeruhiwa vibaya. Usalama umeendelea kusorota Lamu. Kwa mfano, kambi ya jeshi ilivamiwa na magaidi wa Al shaabab. Kwa hivyo, hili ni swala ambalo lazima tuliangalie kwa makini na tuhakikishe kwamba maeneo yote katika Jamhuri ya Kenya ambapo kaunti zinafanya kazi, huduma ya afya zinaboreshwa kuliko zile zinatolewa na hospitali za kibinafsi. Bw. Spika, juzi kulikuwa na mjadala kuhusiana huduma za afya zirudi katika Serikali Kuu au la. Hii ni kwa sababu katika kaunti nyingi, huduma hii imezorota na wananchi wanalalamika kwamba hawapati huduma zinazofaa. Kwa hivyo, lazima Kamati husika ikunje shati na kuhakikisha mambo haya yanachunguzwa na mwafaka unapatikana kuhusiana na swala hii."
}