GET /api/v0.1/hansard/entries/982473/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 982473,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982473/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza ninatoa rambirambi zangu kwa familia ya hayati Mzee Moi na marafiki wao, hususan ndugu yetu Sen. Gideon Moi kwa kumpoteza Mzee . Hili ni jambo la Mwenyezi Mungu na sisi binadamu tunasema analopitisha Mungu hatuwezi kulipinga. Nakumbuka mara ya kwanza kukutana na hayati ilikua mwaka wa 2000 wakati nilikuwa nime chaguliwa kama mwenyekiti wa chama cha wakulima nchini; AgriculturalSociety of Kenya (ASK). Hata wewe Bw. Sipka ulikuwa mmoja wa wanachama wake. Nilikuwa na wasiwasi na tashwishi ya jinsi vile ningeongea mbele ya Rais, maanake ilikua mara yangu ya kwanza kukutana naye. Aliniambia: “Kijana relax, mimi ni binadamu kama wewe, ongea bila wasiwasi wote. Pale utashindwa, nitakusaidia.” Kwa hivyo nilirelax na hatimaye nikaongea na kisha nikamkaribisha ahutubie taifa. Bw. Spika, kifo hiki kimeguza watu wa Kilifi sana. Katika eneo la Kilifi haswa Ganze ambako kila mwaka alikua anaenda kufanya Harambee kusaidia watu walioathirika, shule ama hafla zozote atakazokua amehisia kuzifanya kule. Alikuwa karibu sana na watu wa Kilifi na hatimaye hiyo ilimfanya hata asimame mara ngapi, watu wa Kilifi walikua wanasimama na Mzee Moi. Wakati fulani kulikua na kichekesho fulani cha kusema Moi hasimami safari hii kwa sababu Katiba haimruhusu. Watu walikua wanauliza mbona Moi hasimami? Kwani amekufa? Lakini watu wakasema Katiba imegeuzwa kwa hivyo, haimruhusu lakini hata kama angesimama, bado watu wa Kilifi wangempigia kura. Bw. Spika, la mwisho ni kwamba alikua Mbunge wa Afrika. Nimesikia sifa zote zimetolewa hapa ambazo tunazijua ni kwamba yeye alisaidia mataifa mengine ya Afrika. Mimi kama mwanasiasa mmojawapo wa wale wanasiasa wa Afrika wenye huketi Katika lile Bunge la Afrika, ninataka kwa niaba ya lile Bunge la Afrika nitume rambirambi ya Wabunge wote katika Afrika kwa familia ya Mheshimiwa marehemu Daniel Toroitich arap Moi na watu wote katika familia yao na marafiki zao ili Mwenyezi Mungu airehemu roho yake mahali pema walipo lala wema peponi."
}