GET /api/v0.1/hansard/entries/982481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 982481,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982481/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "ambayo iko karibu na nyumbani kwetu Vanga. Kwa hivyo mimi namkumbuka vizuri Mzee Moi. Pia, alipozungumza Sen. Khaniri hapa, kwetu katika familia ilitufika kwa sababu baada ya babangu kufariki akiwa Mbunge, kakangu aliingia Bunge 1983; marehemu Boy Juma Boy ambaye alikua Seneta Katika awamu ya 2017, Mungu amrehemu na amlaze mahali pema peponi. Mzee Moi alisema anataka kumuona kijana wa Juma Boy anayeitwa Boy Juma Boy na akasimama Boy Juma Boy na tikiti ya KANU kama alivyosema Sen. Khaniri, Mzee akasimama na yeye. Amekua Mbunge wa Kwale Central na Matuga kwa miaka 15. Mwisho nikimalizia, shamba letu la Kwale lilikua linapigwa mnada na Agricultural Finance Corporation (AFC). Hayati Moi akasimamia shamba la babangu likasimama na shamba halikuuzwa. Bw. Spika, Mzee ameondoka lakini twamkumbuka kwa mambo mengi aliyoyafanya. Yangu nikuwaambia Wakenya tumuombee Mungu amlaze mahali pema peponi na ndugu yetu Sen. Moi na ndugu yake Raymond wawe na subra wakati huu. Sisi tuko pamoja. Asante sana Bw. Spika."
}