GET /api/v0.1/hansard/entries/982486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 982486,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982486/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii niweze kutoa rambirambi zangu pamoja na za jamii nzima ya Kilifi. Nakumbuka wakati huo alikua ni mtukufu Daniel arap Moi. Namkumbuka kama jinsi wenzangu walitangulia kusema hasa nitaanza na maziwa nikiwa prefect wakati ule darasani nilikuwa nikihesabu hata wenye hawakuja shule ili yawe mengi na mimi nibebe. Wakati mwingine nilikuwa ninaenda shule hata kama nina homa kwa sababu nimetoka kwa jamii ambayo haijiwezi kiasi kwa hivyo mlo ulikua mmoja na singeweza kukosa shule kwa maana yale maziwa yalikua yananisaidia. Nilikuwa ninaandika wale hawako ili niweze kupelekea wale wenzangu waliokua nyumbani waweze kupata. Katika jamii yangu tumezaliwa watoto wawili, mimi msichana na mwenzangu mvulana ambaye ni mdogo wangu na ako na jina la Moi. Hadi saa hii kuna watu wananitumia rambirambi za pole wakifikiria ni yule kaka yangu. Kwa hivyo kuna machungu fulani ambayo niliyapata kwa kuwa na jina lile la Moi nyumbani. Mwaka wa 1982 nilikuwa bado mdogo lakini nakumbuka kulikuwa na watu waliokuwa wanazunguka wakisema Moi asitajwe. Nilikuwa na shida ya kufanya watoto wasimtaje yule mdogo wangu kwa maana ungemtaja Moi ungeuawa. Wakati huo nilikuwa nang’ang’ana kuhakikisha kwamba watoto wasiliite jina hilo. Ilibidi tumfungie pahali ili watoto wasimwite. Sikujua kilichokuwa kikiendeka wakati huo."
}