GET /api/v0.1/hansard/entries/982490/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 982490,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982490/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Mwaka wa mwisho kuonana na yeye kwa karibu sana nilikuwa Darasa la Nane, mwaka wa 1991. Alikuwa anafungua daraja kule Kilifi. Kama wasichana kuna nyimbo tulimwimbia. Kwa vile kulikuwa na shule moja peke yake katika mji wa Kilifi, tulikuwa tuna msihi tujengewe shule ya wasichana. Baada ya kumwimbia na kumshukuru kwa daraja lile, mwaka uliofuata kuna shule ya wasichana inayoitwa Bahari Girls ilifunguliwa. Hiyo ilikuwa shule yangu ya kwanza kuhudhuria. Kwa hivyo, namkumbuka kwa hilo pia."
}