GET /api/v0.1/hansard/entries/982491/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 982491,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982491/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Wakati alipohudumu kama Rais, kwa mfano, ikiwa Madaraka Day, maduka yote yalikuwa yanafungwa na watu wote walitakiwa kwenda kwa uwanja. Vile vile, kila duka ililikuwa na bendera. Kulikuwa na heshima na hadhi fulani kwa taifa. Kulikuwa na uzalendo na heshima kwa viongozi. Hungemuona kijana akimtukana kiongozi anavyotaka. Hungemdharau kiongozi ama kutumia maneno mabaya."
}