GET /api/v0.1/hansard/entries/982492/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 982492,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982492/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Bw. Spika, hata wakati huu wa mitandao na tarakilishi, heshima na nidhamu ni lazima idumishwe. Nitamkumbuka Mzee Moi kwa heshima kubwa na uzalendo ambao alikuwa ameweka kwa taifa hili. Ukiamka asubuhi, nyimbo zilizokuwa zinakuamsha zilikuwa za uzalendo katika redio zetu. Ulikuwa unahimizwa uamke uende kazini na mambo mengi mazuri ambayo tulikuwa tukiyaona wakati ule. Wakati huu, mazuri mengi yamekuja lakini mabaya pia yamefuata. Ningewahisi tuige kile kizuri na kile kibaya tukiache."
}