GET /api/v0.1/hansard/entries/982518/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 982518,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982518/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "hawakuwa na ile fursa ya kukutana na yeye moja kwa moja. Tulikutana na yeye haswa katika idhaa ya Kiswahili ya Kenya Broadcasting Corporation (KBC). Nakumbuka nilianza kusikia taarifa za habari nikiwa katika shule ya chekechea na tukajua ya kwamba kila wakati taarifa zinaposomwa ni mpaka wahariri wakuu waanze na kueleze pale ambapo Rais wetu alipokuwa. Kwa hivyo, sisi tulimjua. Jina la Moi lilijiandika katika nyoyo zetu. Nakumbuka ya kwamba nikiwa mdogo, tulikuwa tukiuliza: “Na Moi wa Uganda anaitwa nani? Moi wa Tanzania anaitwa nani? Tulifikiria ya kwamba mtu yeyote ambaye ni rais anapaswa kuitwa Moi. Bw. Spika, ninamkumbuka Rais Moi vizuri kwa mambo ya mazingara kwa sababu aliyatilia mkaazo. Nakumbuka miradi ya kuzuia mmomonyoko wa udongo ambayo iliyoongozwa na Mulu Mutyisia. Kwa upande wa elimu, alileta mfumo mpya wa elimu wa 8-4-4 akizingatia kwamba vijana ambao hawakuwa na uwezo mzuri wa masomo pengine walikuwa na talanta au maarifa ya ufundi wangefanya vizuri. Aliyajumuisha vizuri na akaongeza vyuo vikuu hapa nchini kutoka chuo kikuu kimoja na kukawa na vyuo vikuu vingi. Bw. Spika, ninamkumbuka kwa mambo ya elimu, mazingara na pia kwa michezo. Alikuwa akishabikia timu ya Harambee Stars. Nakumbuka nikiwa katika chuo kikuu, tulikuwa tukimngoja pale katika ua kwa sababu tulijua akitoka kushabikia timu ya Harambee Stars, atasimama pale. Kwa sababu ya ukarimu wake, tulimwambia shida zetu. Nakumbuka ya kwamba alituandalia hafla murwa kwa kutupatia chakula. Hiyo ndiyo siku ya kwanza nikiwa chuo kikuu tuliona nyama nyingi na tulikula tukashiba. Bw. Spika, ninamkumbuka kama mtu mkarimu na aliyejitolea. Kwa upande wa ufisadi, alijitolea mhanga kupigana na ufisadi. Mswahili anasema ya kwamba hakuna mtu asiye na kasoro ila Mwenyezi Mungu. Yeye alikuwa na upungufu wake. Kile ambacho kimebaki ni kuwa tunapaswa kusoma ni ile filosofia ya Nyayo – Amani, Upendo na Umoja. Tukizingatia hayo, Kenya itakuwa moja. Tutasonga mbele tukiwa kitu kimoja na Kenya itaendelea kutoka hatua moja mpaka nyingine. Najua hilo ndilo jambo muhimu alilotuachia kama nchi. Asante sana, Bw. Spika."
}