GET /api/v0.1/hansard/entries/982713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 982713,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982713/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "South Imenti, Independent",
"speaker_title": "Hon. Kathuri Murungi",
"speaker": {
"id": 2802,
"legal_name": "Kathuri Murungi",
"slug": "kathuri-murungi"
},
"content": " Ahsante sana, Bwana Spika. Kwa niaba ya wakaazi wa Eneo Bunge la Imenti Kusini, familia yangu na mimi mwenyewe, nachukua fursa hii kuomboleza kuachwa na Baba Moi. Rais Moi alifanya mambo mengi sana hapa nchini Kenya kwa mfano elimu na hasa kusimamia demokrasia kwa kukubali kuondolewa kwa Kifungu cha 2A cha Katiba yetu, pamoja na vile alivyopeana uongozi. Wakenya wengi walifikiria hataachilia uongozi sababu alikuwa Rais kwa miaka 24 na Naibu wa Rais kwa miaka minane. Sisi kama viongozi tunaiga mfano wake na kuombea familia yake na Wakenya wote wakati mwema tunapomlaza Rais Moi wiki hii."
}