GET /api/v0.1/hansard/entries/982834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 982834,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/982834/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Asante Mhe. Spika. Nasimama kutoa rambirambi zangu binafsi, za familia yangu na za watu wa Wundanyi na Taita/Taveta kwa jumla kwa kumpoteza aliyekuwa Rais wa nchi hii, hayati Daniel Toroitich arap Moi. Nilifaidika sana na Maziwa ya Nyayo. Kwenda shule Jumatatu, Jumatano na Ijumaa wakati ule ilikuwa ni lazima kwa sababu tulipewa maziwa siku hizo. Mpaka nilipokuwa mtu mzima, sijaona maziwa yaliyo na kile kwa Kiingereza kinaita ‘cream’. Ilikuwa unapasua lile boksi ukimaliza kunywa maziwa unapata ‘cream’ nzuri sana. Naomba mwenyezi Mungu alaze roho yake mahali pema peponi."
}