GET /api/v0.1/hansard/entries/983004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 983004,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/983004/?format=api",
    "text_counter": 413,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nominated, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Halima Mucheke",
    "speaker": {
        "id": 13169,
        "legal_name": "Jeniffer Shamala",
        "slug": "jeniffer-shamala"
    },
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii kuliwaza familia ya marehemu aliyekuwa Mtukufu Rais wa pili, Daniel Toroitich arap Moi. Namkumbuka marehemu kwa mambo matatu. La kwanza, nilifaidika na maziwa ya bure. Pili, wakati nilikuwa katika shule ya upili, alipitia shuleni kwetu na tulipoenda kumwimbia, alinipa kifurushi cha pesa ambacho nilipeleka shuleni tukachinjiwa ng’ombe na tukanywa soda. Hayo mambo yalinifanya nimpende sana Rais Moi na kumkumbuka siku nyingi kwa sababu wakati huo, shule nzima ilinisalimia ili wasikie mguzo wa mkono wa Rais."
}