GET /api/v0.1/hansard/entries/983107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 983107,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/983107/?format=api",
    "text_counter": 516,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi South, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": " Kwa niaba yangu na watu wa Kilifi South, nachukua nafasi hii kutoa rambirambi zangu za dhati kwa jamaa na marafiki wa mwenda zake Rais Moi. Ninakumbuka msemo mmoja wa mzungumzaji Albert Einstein. Alisema kwamba mtu ambaye hajafanya kosa ni yule hajajaribu kufanya kitu chochote. Kwa hivyo, katika mazungumzo yake, mheshimiwa aliyeenda zake alisema yuko tayari kusamehe mtu yeyote aliyemkosea na yeye pia akaomba msamaha kwa aliowakosea. Nina imani maombi hayo yametufikia. La mwisho ni kwamba Rais wetu ameenda akiwa na ndoto ambayo haijatimia. Alianzisha mpango wa kutengeneza gari. Ameenda kama ndoto ile haijatimia. Tusipate laana wala dua, tuhakikishe Wakenya tunaendeleza ndoto hiyo."
}