GET /api/v0.1/hansard/entries/983912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 983912,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/983912/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kuairishwa kwa Seneti kama ilivyokarabatiwa na Seneta Ochilo-Ayacko. Kwanza, ningependa kuipongeza Serikali kwa kuwa wazi kwamba janga la Corona limefika katika nchi yetu ya Kenya, na kwamba, tayari tunawaathiriwa wanne ambao wameweza kutambuliwa na kuwekwa katika quarantine. Pili, kule Kaunti ya Mombasa siku ya Jumamosi, tulikuwa na mkutano uliosimamiwa na Gavana wa Kaunti ya Mombasa na vilevile Kaunti Kamishna wa Mombasa ili kuweka mikakati ya kupambana na janga hili la Corona. Jambo la kufurahisha ni kuwa, tayari Kaunti ya Mombasa tumejitayarisha na tuna vyumba maalumu ambavyo vimetengwa katika hospitali kuu ya Coast General. Vile vile, kuna hospitali mbili mpya zimejengwa lakini bado hazijawekwa vifaa vinavyoweza kutumika kama mahali ambapo wale wagonjwa wa Corona wanaweza kuwekwa ili waweze kutotangamana na wagonjwa wengine. Bi. Spika wa Muda, maandalizi yetu yako sawa isipokuwa tuna tatizo la feri. Kwa sababu kama unavyojua, kivukio cha Feri ya Likoni kinahudumia wakaazi laki tatu kwa siku. Kwanzia saa kumi na mbili ama saa kumi na moja alfajiri hadi saa tano usiku wanaotumia kivuko kile ni zaidi ya watu laki tatu. Vile vile, magari zaidi ya elfu tatu yanatumika katika kivuko kile. Bi. Spika, wa Muda, jambo la kusikitisha ni kwamba, katika feri ile, mbali na kuwa kuna msongomano, hatujakuwa na mikakati yoyote ya kuhakikisha ya kwamba, wananchi walioko pale wako salama. Ijapokuwa mkutano wa juzi ulipitisha kuekwe maji ya kuosha mikono na sabuni na vile vile vifaa vya sanitizer. Jambo hilo halijatekelezwa kwa sababu ya ukosefu wa hela. Bi. Spika wa Muda, huduma za feri bado ziko katika mikono ya Serikali ya kitaifa. Bunge la Seneti linafaa kupeleka malalamiko kwa Serikali ili kuhakikisha kwamba feri zinaangaliwa. Hii ni kwa sababu huduma za feri ni kiunganishi baina ya Kenya na nchi jirani ya Tanzania. Jana Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Tanzania alitangaza kwamba ugonjwa huo pia umefika nchini Tanzania. Kwa hivyo, ipo hatari kubwa ya wagonjwa kupitia mpaka wa Lunga Lunga na mipaka mingine kupitia kivuko cha feri. Katika feri, watu huwa wako bumper to bumper kama wanavyosema wataalamu. Hakuna nafasi. Kuna feri ambazo huvukisha raia wakati watu ni wengi, haswa jioni. Kwa hivyo, kuna hatari kubwa ya wananchi kuambukizwa ugonjwa huo. Itabidi Serikali iangazie jambo hilo kwa haraka. Hakuna haja ya kupanga mikakati mingine wakati hatujashughulikia sehemu nyingine ambazo ni hatari zaidi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}