GET /api/v0.1/hansard/entries/983925/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 983925,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/983925/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii na hasa mabadiliko yaliyopachikwa na Seneta wa Migori. Bi. Spika, kwa kweli, tangu ugonjwa wa (COVID-19) utangazwe kote duniani, hapa Kenya watu wamepata wasiwasi mwingi sana. Kuna uvumi mwingi unaendelea hapa na pale. Mimi naonelea kwamba ni bora Seneti isiairishe vikao vyake kwa sababu wananchi wa Kenya wako na imani sana na Bunge la Seneti. Wanapoona Bunge la Seneti liinahairisha vikao vyake, hofu yao itaongezeka maradufu. Kwa wakati huu ambao tunaenda nyumbani, hata wale ambao wako katika kaunti ambazo sisi tunarudi wanajuwa hii ugonjwa bado haijafika huko Taita Taveta, Tana River na sehemu za chini. Lakini habari wanayopata ni kwamba, huko Nairobi ndiyo watu wamepatikana wakiwa na huo ugonjwa, hasa wale waliosafiri kurudi upande huu. Bi Spika wa Muda, huko Kaunti ya Tana River, siku hizi watu huulizana, ni watu wangapi wametoka Kaunti ya Jiji la Nairobi. Sisi tukienda tuongezeke huko, watasema tumetoka sehemu ya magonjwa. Kwa vile Hoja imetolewa na pia mabadiliko kuwekwa, sina budi kuunga mkono. Hoja inasema tuende mapumziko kwa majuma mawili. Tutakaporudi, tutakaa siku moja moja kwa majuma mengine mawili yatakayofuatia ili tuzungumze yatakayojiri."
}