GET /api/v0.1/hansard/entries/983926/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 983926,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/983926/?format=api",
    "text_counter": 291,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Kwa kweli, kama leo hatungeairisha kikao chetu, tungekuwa tunafuatilia wenzetu ambao tayari wameambukizwa, na kama idadi hii itaongezeka au kupungua kwa wale walio hospitalini. Kwa walio hospitalini, tunawaombea Mungu, wapate afueni ya haraka na watoke hospitalini. Wakati huu ambao tutaenda nyumbani, tutaenda kuangalia mikakati iliyowekwa katika kaunti ambayo itasaidia kupunguza maambukizi zaidi kwa wakati huu."
}