GET /api/v0.1/hansard/entries/986418/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 986418,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/986418/?format=api",
"text_counter": 78,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Ninampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kwa taarifa hii nzuri. Kwanza kabisa, jambo la kuwazuia wagonjwa katika hospitali limekuwa mazoea. Ukiangalia malipo yanayotozwa hospitalini baada ya yule mgonjwa anapokufa, unapata kwamba ni hela ambazo kwa ukweli hazina maana yoyote. Kwa mfano, sindano inayouzwa kwa Kshs3 unapata inauzwa kwa Kshs300 ili ada ya hospitali iwe kubwa hadi anashindwa kulipa. Ikiwa mgonjwa amekufa, ada ambayo familia yake inatozwa inaongezeka marudufu. Unashindwa hii ni nchi gani. Jambo lingine ambalo lina nishtua zaidi ni kwamba Mwenyekiti hangekuja kusema anataka taarifa yenyewe. Mwenyekiti angekuja katika Bunge hili na kutuelezea mambo ambayo Kamati ya Afya imefanya na kupendeza majibu. Hangepaswa kuja kuuliza. Angekuja kutuambia nimefanya hili na pahali ambapo inaleta kizungumkuti ni hapa ili tuweze kumsaidia. Lakini yeye kuja katika Bunge la Seneti---"
}