GET /api/v0.1/hansard/entries/986429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 986429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/986429/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Nilianza kwa kusema kwamba, nampongeza Mwenyekiti wangu kwa kuwasilisha taarifa nzuri sana katika Bunge hili la Seneti. Nina uhakika kwamba wenzangu hawakunielewa kwa sababu nilitumia lugha ya Kiswahili. Wakati mwingine nitatumia lugha ya Kiingereza kwa sababu wamebobea kwa lugha hiyo sana. Bw. Spika, ninasema kwamba, tabia ya hospitali kuwazuilia wagonjwa kwa sababu ya kutolipa ada ya hospitali haikubaliki. Jambo ambalo nilikuwa na shida nalo ni kwamba Mwenyekiti wangu angekuja katika Bunge la Seneti na kutueleza hatua ambazo Kamati yake imechukua kutatua tatizo hilo. Sikusema ni makosa yoyote. Nimesema kwamba, ninampongeza kwa taarifa hiyo. Pengine ningeongea kwa lugha ya Kiingereza, Sen. Ledama na Sen. Cherargei wangenielewa zaidi."
}