GET /api/v0.1/hansard/entries/986526/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 986526,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/986526/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa hii fursa kuungana na Maseneta wenzangu kumshukuru Kiongozi wa Wengi kwa Taarifa aliyotupa kuhusu janga liliotokea katika kaunti za Elgeyo-Marakwet na Pokot ya Magharibi. Tunaomboleza wale ambao walipatwa na janga hili. Tunaomba Serikali ijizatiti na kusaidia walioathirika. Wapewe chakula na nyumba. Serikali inaweza kutengeneza hema ili wale wananchi wasiendelee kuteseka. Wengi wa wale walioathirika sana ni watoto na akina mama. Kusema kweli hatuko sawa sana katika muundo wa sheria hapa nchini. Ninajiunga na akina Sen. Sakaja na wengine kusema kwamba kuna njia tunaweza leta muundo wa kisheria wa kusimamia majanga hapa nchini. Pia nakubaliana na wenzangu kwamba wengi wa wale ambao wameathirika watahitaji huduma za kiafya. Watibiwe bila"
}