GET /api/v0.1/hansard/entries/986530/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 986530,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/986530/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omanga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13175,
"legal_name": "Millicent Omanga",
"slug": "millicent-omanga"
},
"content": "Asante, Bw Spika. Ningependa kutoa rambirambi zangu kwa familia za West Pokot na Elgeyo-Marakwet ambao walipatwa na janga hili la mafuriko. Kabla kuja hapa, niliona kwenye televisheni katika habari za mchana, kwamba hata kule Trans Nzoia kuna daraja ambazo zimeanguka kwa sababu ya mafuriko. Vile vile katika Kaunti ya Kericho kuna mafuriko. Kule Ahero katika Kaunti ya Kisumu, watu wamehama na mizigo yao na sasa wako barabarani wanangoja wapelekwe mahali salama. Mafuriko yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuna sehemu ambazo hazikosi kufurika kama vile Murang’a. Kama Seneta mwenzangu kutoka Taita-Taveta alivyosema, pia kaunti za Tana River na Taita-Taveta hufurika mara kwa mara. Sasa hivi kuna sehemu zinazoathirika kutokana na mafuriko. Tunafaa kutafuta suluhu ya kudumu. Sisi Maseneta tumesema kuwa tutasaidia watu wa West Pokot na Elgeyo-Marakwet. Hata hivyo, hatuwezi kufaulu pekee yetu. Tunafaa kuwa na sheria na mikakati ya kusaidia watu mafuriko yanapotokea. Nikiwa ningali ninasoma, aliyekuwa rais, hayati mzee Moi, alipenda kuzungumza kuhusu mmomonyoko wa udongo. Alitaka watu kupanda miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo. Kwa hivyo, tunafaa pia kuwarai wananchi wenzetu kuendelea kupanda miti. Tuwache kukata miti ili kuzuia mafuriko na mmomonyoko wa udongo. Asante, Bw. Spika."
}