GET /api/v0.1/hansard/entries/987999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 987999,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/987999/?format=api",
"text_counter": 1253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Asante, Mhe. Spika. Kwanza nashukuru umenipa nafasi. Mimi ni mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Bajeti na Makadirio. Kwa kweli, tumekuwa na kipindi kizuri cha kuangalia hesabu iliyotolewa kutoka Hazina ya Kitaifa. Mapema leo hii tulipata nafasi kuangalia ripoti ya Kamati ya Hazina. Sasa tumepata nafasi nzuri tena ya kujadili Mswada huu wa Makadirio ya Ziada."
}